WALIMU WA VYUO VYA HABARI WAPEWA SOMO

Walimu ambao wanafundisha kwenye vyuo vinavyotoa taaluma ya habari wameshauriwa kuwatembelea wanafunzi ambao wapo kwenye mafunzo ya vitendo (field) ili kufahamu maendeleo yao.

Wito huo umetolewa jana na ndugu Keny Mahondo msimamizi wa vipindi Country Fm radio iliyopo katika jengo la chama cha walimu mkoani Iringa alipokua akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha uandishi wa habari Time School Journalism (TSJ) walipokwenda kufanya ziara ya kimasomo kwenye radio hiyo.

Mahondo aliseama walimu ambao wanafundisha kwenye taasisi  zinazotoa taaluma ya habari wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kuwatembelea wanafunzi wao ambao wapo kwenye vituo vya mafunzo ili kufahamu maendeleo yao kuliko kukaa na kuwasubiri wamalize mafunzo na kurudisha ripoti vyuoni.

"Ni vyema walimu wakawa na utaratibu wa  kuwatembelea wanafunzi ambao wapo kwenye mafunzo ya vitendo walau mara moja ili kujua maendeleo yao na pia kufahamu kama wanatimiza kile kilichowapeleka" Aliseama Mahondo.

Pia ndugu Mahondo aliwashauri wanafunzi ambao wanachukua taaluma ya habari kujituma zaidi hususani wanapouka kwenye mafunzo ili kuweza kujitengenezea nafasi za kupata ajira katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.

Wanafunzi wa (TSJ) wakiambatana na baadhi ya walimu wao wamefanya ziara ya siku tatu mkoani Iringa na kutembelea sehemu mbalimbali za kihistoria za mkoa huo kama vile eneo la kihistoria la kalenga, makumbusho ya zama za mawe ya Isimila (Isimila stone age site) pamoja na eneo la la maajabu la Mkwawa (Mkwawa magic site).

Msimamiza wa vipindi wa country Fm radio  Keny Mahondo (kulia) akizungumza
na baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha uandishi wa habari TSJ (hawapo pichani) walipokwenda kufanya ziara ya kimasomo kwenye radio hiyo jana kushoto ni mfanyakazi wa country Fm radio  Kelvin Lameck.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha uandishi wa habari TSJ wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa country Fm radio walipokwenda kufanya ziara ya kimasomo kwenye radio hiyo Jana.

No comments: