UTARATIBU WA KUHIFADHI MAENEO YA KIHISTORIA BADO NI CHANGAMOTO

TanzanianTanzania ni moja kati ya nchi zenye vivutio vingi vya asili vya kitalii duniani, inashika nafasi ya pili kwenye orodha ya nchi zinazoongoza kwa vivutio hivyo  nyuma ya nchi ya Brazil ambayo inashika nafasi ya kwanza.

Vivutio kama vile maeneo ya kihistoria, mbuga za wanyama, milima, mito pamoja na maziwa vimekua vikichangia kwa kiasi kikubwa katika kuongeza pato la taifa.

Moja kati ya changamoto kubwa ambayo inaikumba nchi yetu ili kuhakikisha vivutio hivyo vinadumu kwaajili ya matumizi ya vizazi vijavyo ni swala zima la uhifadhi na utunzaji wa vivutio hivyo.

Akizungumza hivi karibuni na wanafunzi wa Chuo cha uandishi wa habari Time School of Journalism (TSJ) walipokwenda kufanya ziara ya kimasomo katika makumbusho ya ngome ya Chief Mkwawa yaliyopo eneo la Kalenga mkoani Iringa msimamizi wa eneo hilo ambae alikua ndio kiongozi wa ziara hiyo (Tour guide)  Zuberi Suleiman Mwawitala alisema uhifadhi na utunzaji wa maeneo ya kihistoria hususani eneo la ngome ya Chief Mkwawa umekua ni changamoto kubwa sana kwani wanafamilia wa Mkwawa ndio hasa wanaofanya kazi ya kuhifafhi eneo hilo.

"Changamoto ambayo ni kubwa katika eneo hili ni uhifadhi pamoja na usimamizi wa eneo hili kwani wanafilia wa Mkwawa ndio wenye jukumu la kutafuta pamoja na kuhifadhi vitu vyote vinavyohusu historia ya Chief Mkwawa kama vile fuvu na vitu vingine" Alisema Mwawitala.

Aidha Mwawitala alisema mwaka 2014 wajerumani walikuja katika eneo la ngome ya Chief Mkwawa kwaajili ya kulirudisha jino la Chief Mkwawa ambalo walikaa nalo kwa zaidi ya miongo minne kutokakana na jino hilo kuwasumbua na kudai kurudi nyumbani.

Katika ziara hiyo wanafunzi wa TSJ waliweza kujioneo vitu mbalimbali katika eneo hilo kama vile fuvu la Chief Mkwawa, bunduki iliyotumika kumuulia Chief Mkwawa, silaha za jadi alizotumia Chief Mkwawa pamoja na makaburi ya wanafamilia wa Chief Mkwawa.

Zuberi Suleiman Mwawitala akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha uandishi wa habari TSJ nje ya jengo la makumbusho ya mtemi Mkwawa eneo la Kalenga mkoani Iringa hivi karibuni

Jengo  linalotumika kuhifadhia vitu mbalimbali vya historia ya mtemi Mkwawa ( Mkwawa museums)  lililopo Kalenga mkoani Iringa.

No comments: