Kuna msemo
wa kiswahili unaosema, hakuna lenye mwanzo linalokosa mwisho, zimebaki siku chache ili mwaka 2015
uweze kufika mwisho na hatimaye kuukaribisha mwaka mpya wa 2016.
Mwaka 2015
umekuwa wa kihistoria kwenye nchi ya Tanzania, kwavile ulisheheni matukio
mbalimbali ya kufurahisha pamoja na kusikiktihsa,matukio ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni
pamoja na kimichezo yaliweza kujitokeza hapa nchini.
Tukiwa
tunaelekea kuumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016, makala hii
inakuletea matukio mbalimbali ya kimichezo yaliyojitokeza mwaka huu na kuteka
hisia za wanamichazo wengi nchini
Tanzania.
Kichapo cha magoli 7-0 ilichokipata
Tanzania dhidi ya Algeria
Baada ya
kufanikiwa kuitoa timu aya taifa ya Malawi kwa ushindi wa jumla wa mabo 2-1, kwenye
mechi ya raundi ya kwanza kufuzu hatua ya makundi, kuwania tiketi ya kushiriki
fainali za kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika mwaka 2018 nchini Urusi,
timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ilikutana na timu ya taifa ya Algeria.
Kwenye mechi
ya kwanza iliyopigwa kwnye uwanja wa taifa jjini Dar es salaam, timu hizo
zilitoka sare ya mabao 2-2, mabao ya stars yakifungwa na Elias Maguri na Mbwana
Samata, huku yale ya kusawazisha ya Algeria yakifungwa na Islam Sliman.
Wiki moja
baadae Stars walisafiri kwenda nchini Algeria kucheza mechi ya marudiano na
mbweha hao wa jangwani, na kushuhudia stars
wakipokea
kipigo cha fedheha cha bao 7-0. Kwa matokea hayo Stars ilisukumizwa nje ya
mashindano hayo kwa jumla ya mabao 9-2.
Matokeo hayo
yaliwashtua sana wapenzi wengi wa soka hapa nchini kutokana na kiwango
walichokionyesha Stars kwenye mechin ya kwanza hapa nyumbani.
“Kwakweli
sikutegemea tungefungwa idadi hiyo ya mabao, kwa jinsi timu ilivyocheza mechi
ya kwanza hapa nyumbani , wachezaji walionyesha kujituma na kujiamini sana na
kutawala mchezo vizuri. Lakini ndio mpira jinsi ulivyo kilichobaki ni kuangalia
mashindano mengine,” aliseama Frank William shabaiki wa soka kutoka maeneo ya
kinondoni.
Kukamilika kwa mradi wa kituo cha
michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park.
Mwezi Oktoba
mwaka huu aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete alizindua kituo cha
michezo cha Jakaya Kikwete Youth Park kilichopo eneo la kidongo chekundu jijini
Dar es salaam, kilichojengwa na kampuni ya umeme ya Symbion Power kwa
kushirikiana na klabu ya Sunderland inayoshiriki ligi kuu ya England.
Dk Kikwete
alikubali kuzindua kituo hicho wakati wa mazungumzo kati yake na mtendaji mkuu
wa Symbion Power, Paul Hinks kwenye hotel ya JW Marriot Essex House mjini New
York nchini Marekani, ambako Rais huyo mstaafu alipokuwa anafanya ziara ya
kikazi nchini humo.
Hinks
alimueleza Dk kikwete kuwa ujenzi wa kituo hicho umekamilika tayari kwa
uzinduzi na hivyo kuongeza thamani kubwa kwenye eneo ambalo zamani lilkua
gereji ya kutengeneza magari.
Kituo hicho
kimegharimu kiasi cha Dola za kimarekani milioni mbili na ni matokeo ya
ushirikiano wa kampuni ya Symbion Power ya Marekani, klabu ya soka ya
Sunderland inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza na taasisi ya Grasshopeper Soccer
ya nchini Australia.
Kituo hicho
kitatumika kuendeleza vipaji kwa vijana wenye umri chini ya miaka 10 katika
michezo kama mpira wa miguu, mpira wa
magongo pamoja na kakapu.
Samata, Ulimwengu waweka rekodi
Nyota wa kimataifa
wa Tanzania mbwana Samata, alifunga goli moja kwenye ushindi wa magoli 2-0,
iliyoupata timu yake na Tp Mazembe kwenye mchezo wa marudiano wa fainali ya
klabu bingwa Afrika dhidi ya Usm Alger, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Stade
TP Mazembe mjini Lubumbashi, Jamhuri ya Kdemikrasia ya Kongo.
Goli hilo
lilimfanya Samata kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo kwa kufikisha jumla ya
magoli 8, akimpiku Bakryu’Al Medina wa El Merekh aliyefunga jumla ya magoli 7 ambaye alikua
akichuana nae kwa karibu.
Samata na
Ulimwengu wameweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kunyanyua kombe la klabu
bingwa Afrika, huku nyota wengine waliong’ara kwenye medani ya soka wakishindwa
kufanya hivyo.
Kwa upande
wake Samata ameweka rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kunyakuwa tuzo ya
mfungaji bora wa michuano ya klabu bingwa Afrika.
Wachezaji
hao pia wameweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kucheza michuano ya klabu
bingwa ya dunia yanayoendelea nchini Japani.
Azam yaweka rekodi kombe la Kagame
Azam Fc
iliwatoa kimasomaso watanzania baada ya kufanikiwa kutwaa kombe la klabu bingwa
Afrika mashariki na kati (Kagame) kwa kuilaza timu ya Gor mahia ya Kenya kwa
mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Ubingwa huo wa Kagame ni wakwanza kwenye historia ya klabu
hiyo baada ya kufanikiwa kuchjeza fainali mbili, fainali ya kwanza walicheza
mwaka 2012 dhidi ya klabu ya Yangana kupoteza kwa magoli 2-0, na mwka huu
wameingia katik historia ya vilabu vilivyofanikiwa kulitwaa kombe hilo.
Kitu cha
kufurahisha na chakukumbukwa katika michuano hiyo ni baada ya Azam kutwaa
ubingwa huo bila Kurusu wavu wao kuguswa, ukiacha magoli matatu waliyofungwa na
Yanga wakati ikitoka na ushindi wa matuta 5-3 kwenye hatua ya robo fainali.
Kwa ubingwa
huo klabu hiyo ilifanikiwa kuondoka na kitita cha Dol za kimarekani elfu 40,
mshindi wa pili timu ya Gor mahia ilipata Dola elfu 25 na mshindi wa tatu klabu
ya KCCA ya Uganda ikipata Dola za kimarekani elfu 10.
Vodacom wasaini mkataba mpya na TFF
kwaajili ya udhamini wa ligi kuu bara
Shirikisho
la mpira wa miguu Tanzania TFF mwaka huu lilisaini mkataba mpya wa miaka mitatu
na kampuni ya simu za mikonni ya Vodacom kwaajili ya udhamnini wa ligi kuu
Tanzania bara.
Mkurugenzi
wa mawasiliano na masoko wa Vodacom Kelvin Twise alisema mkataba huo unaongezeko
la aslimia 40 kutoka kwenye udhamini wa miaka iliyopita ambapo udhamini ulikuwa
ni Tshs 1.6 bilioni na mkataba wa sasa utagharimu Tshs 2.3 bilioni.
Twise
aliongeza kuwa ongezeko kubwa la udhamini limekwenda katika usafiri wa timu kwa
sababu timu nyingi zimekuwa zikilalamika kuwa zinapata wakati mgumu kwenye gharama
za usafiri, kwahiyo katika fedha hiyo ya udhamini kiasi cha Tshs 1.2 bilioni
zitakwenda kwenye timu zote 16, waamuzi wanagharimu zaidi ya milioni 360,
maafisa wengine wa mechi ambao wanakuwa nje ya uwanja wanagharimu zaidi ya milioni 62,TFF wanapata
milioni 183 na zawadi zitagharimu milioni 174.
Ziara ya magwiji wa klabu ya
Barcelona .
Mashabiki wa
soka nchini mwaka huu walipata nafasi ya kuwashuhudia magwiji wa klabu kubwa
Duniani ya FC Barcelona ya nchini Hispania wakiwemo PatrickKluivert, Gazka
Mendieta, Anderson De Souza maarufu kama Deco, Francesco Cocu na Luis Garcia
walipofanya ziara ya kimichezo mapema mwka huu.
Kwenye ziara
hiyo magwiji hao walifanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya kitalii nchini na
kupata nafasi ya kucheza mechi ya kirafiki na magwiji wa Tanzania mchezo
uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Hii ilikuwa
ni mara ya pili kwa magwiji wa klabu kubwa za nchini Hispania kufanya ziara
nchini baada ya magwiji wa klabu ya Real Madrid kufanya ziara kama hiyo mwaka
uliopita.
Kikosi cha
magwiji hao wa Barcelona kilisheheni wachezaji wengi waliotamba kipindi cha
nyuma, mbali na Kluivert na wengine ambao mashabiki wengi walikuwa na shauku ya
kuwaona pia walikuwepo magwiji wengine waliokuja kwnye zira hiyo chini ya kocha
maarufu na kiungo nyota wa zamani wa klabu hiyo mholanzi Johan Cruyff.
Ziara hiyo
ilikua na manufaa makubwa kwa nchi ya Tanzania katika Nyanja tofauti kama vile
utalii,biashara pamoja na kuanziahsa mahusiano ya kimichezo baina ya klabu hiyo
na Tanzania, uhusiano ambao utafungua milango kwa watanzania wenye vipaji vya
soka kuapata nafasi ya kwenda kufanya majaribia kwenye klabu hiyo.
Startimes, Sahara Media wadhamini ligi daraja la kwanza Tanzania bara.
Kapuni ya
Startime ilisaini mktaba wa mika mitatu n shirikisho la soka Tanzania (TFF),
kwaajili ya udhamini wa ligi daraja la kwanza Tanzania bara wenye thamani ya
Tshs milioni 900.
Akizungumza
jijini Dar es salaam wakati wa kusaini kataba huo, mkurugenzi wa Startimes, Langfang Liao alisema lengo la
kudhamini ligi hiyo ni kusaidia kuendeleza soka la Tnzania liweze kufahamika na
kuonekena moja kwa moj katika chaneli za startimes barani Afrika.
TFF pia
iliingia mktaba na kampuni ya Sahara Media Group kupitia chaneli yake ya Star
TV wenye thamani ya shilingi milioni 450, kwaajili ya kurusha matangazo ya ligi
hiyo nchni.
Udhamini wa
kampuni hizo utasaidia ligi hiyo kupunguza changamoto zianazoikabili kama vile
vilabu vya ligi hiyo kukosea pesa za usafiri pamoja na malipo ya wachezaji.
Mkwasa apewa shavu Stars
Juni 23
mwaka huu shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF lilimpatia mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba mosi 2015 na kumalizika Machi 31 ,2017 kocha wa sasa wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa
stars) Charles Boniface Mkwasa kukinoa kikosi hicho.
TFF ilifikia
makubaliano hayo na Mkwasa baada ya kuridhika na utendji wake katika kukinoa
kikosi hicho kama kocha wa muda, ambapo mpaka kipindi hicho alifanikiwa
kuiongoza Stars katiaka michezo miwili dhidi ya Uganda na Nigeria ambayo yote
iliisha kwa sare.
Hatua hiyo
ilikuja baada ya TFF kusitisha mkataba wake na aliyekuwa kocha mkuu wa timu
hiyo Mholanzi Martin Noij baada ya kutoridhishwa na wa timu apmojana matokeo,
ikiwemo kupoteza michezo mitatu ya Cosafa dhidi ya Swatziland, Madagascan a
Lesotho pamoja na mchezo wa kuwania kufuzu faianali za AFCON dhidi ya Misri.
Mkwasa ambae
kabla kupewa kazi ya kuionoa Stars alikua kocha msaidzi wa klabu ya Yanga,
anakuwa kocha wa kwanza mzawa ndani ya kipindi cha zaidi ya miakani 10
iliyopita kupatiwa mkataba wa kuwa kocha mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa,
baada ya kushuhudia makocha wa kigeni wakina,Marcio Maximo,Kim Poulsen na
Martin Noij wakifundisha bila mfanikio yaliyokusudiwa.
Matumla(Junior), amtandika mchina
Mwaka huu
bondia wa Tanzania Mohamed Matumla (Snake Jonior), aliwakosha wapenzi wa mchezo
wa masumbwi waliohudhuria mpambno mkali na wakusisimua ndani ya ukumbi wa
Diamond Jubilee baada ya kumshinda kwa pointi bondia kutoka China Wan Xin Hua,
kwenye pambano la raundi 10 Machi 28 mwka huu.
Baadhi ya
mashabiki waliojitokeza kwenye usiku huo maalumu uliopewa jina la ‘Night of
Knockout’ kushuhudia mpambano huo, wakiwemo wasanii kutoka tasnia mbalimbali
hapa nchini pamoja na wapenzi wengine wa mchezo huo, walielezea uzuri wa
pambano hilo ambalo lilivuta hisia za wanamichezo wengi hapa nchini hususani
wapenda masumbwi.
“Mimi
binafsi sijawahi kuhudhuria mapambano ya ngumi, lakini leo nafikiri ndio
itakuwa muendelezo wa kuhudhuria mapambano kama haya, kiukweli nimefurahi sana
sjawahi kuamini kama kuna mtu anaweza akapigwa hadi akalala chini na kuendelea
tena, ila leo nimejionea mwenyewe “,alisema Shetta msanii wa muziki wa kizazi
kipya nchini alipohojiwa na waandishi wa habari mara baada ya pambano hilo.
Simba yavunja mwiko Mkwakwani
Klabu ya
wekundu wa msimbazi Simba kwa mara ya kwanza ilifanikiwa kuvuna pointi 6 kwenye
dimba la mkwakwani Jijini Tanga baada ya kufanikiwa kupata ushindi kwenye mechi
mbili mfululizo katiaka uwanja huo.
Mabingwa hao
wa zamani wa ligi kuu Tanzania bara,
walivunja mwiko huo baada ya kuzifunga timu za Afrikani sports 1-0 na Mgambo
JKT kwa jumla ya mabao 2-0.
Simba vs Mgambo
Toka klabu ya Mgambo JKT ipande ligi
kuu soka Tanzania bara msimu wa 2012/2013 imekutana na Simba mara 4.
Imeshinda mara 1, imefungwa mara mbili
na kutoa suluhu mara 1.
Oktoba 21 mwaka 2012 uwanja wa CCM
Mkwakwani Tanga, Mgambo JKT ilitoka suluhu (0-0) na Simba. Mechi ya marudiano
uwanja wa Taifa, Dar es salaam, Mei 8, 2013, Simba ikashinda 1-0.
Msimu uliofuata (2013/2014) Simba chini
ya Abdallah Kibadeni, septemba 18 mwaka 2013 iliishindilia Mgambo JKT 6-0
Uwanja wa Taifa Dar es salaam. Mechi ya marudiano Mkwakwani Tanga, Mgambo
ikashinda 1-0 na ilikuwa februari 9 mwaka 2014.
Matukio
ya Juma Nyosso.
Kwa mashabiki wa soka nchini waliofuatilia
ligi kuu bara msimu wa 2014/15 wataendelea kukumbuka tukio la udhalilishaji lililofanywa
na beki mahiri wa klabu ya Mbeya city inayoshiriki ligi hiyo Juma said Nyosso.
Nyosso alimshika makalio, aliyekuwa mshambuliaji
wa Simba Elias Maguri wakati wa mechi ya ligi hiyo baina ya Mbeya city dhidi ya
Simba, baada ya tukio lile Nyosso aliomba radhi kwa kamati ya maadili ya TFF na
kuahidi kuwa hatorudia tena kufanya hivyo.
Mwaka huu kwenye mchezo wa ligi kuu
Tanzania bara msimu wa 2015/16 kati timu yake dhidi ya Azam FC Nyosso alirudia
tukio lilelile kwa mshambuliaji na nahodha wa klabu ya Azam John Bokko.
Tukio hilo lilionekana kuwachukiza
wapenda soka wengi hapa nchini hususani wanaofuatilia ligi kuu bara ukizingatia
kuwa alishaahidi kuwa hataruidia kufanya tena .
“Kitendo kilichofanywa na Juma Nyoso ni cha kulaaniwa na kupigwa vita
kwasababu kinaharibu maana halisi ya mchezo wa soka ambao ni wa kistaarabu
unaochezwa na waungwana wapenda amani lakini kwa beki huyu wa Mbeya City haiko
hivyo,” alisema Kheri Mlangwa shabiki wa soka kutoka Temeke.
Baada ya tukio hilo kamati ya uendeshaji wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania,ilitangaza kumfungia kwa miaka miwili na faini ya Sh. Milioni
2,Nahodha huyo wa Mbeya City kwa kitendo hicho cha udhalilishaji.
No comments:
Post a Comment