Watumishi wa
jeshi la magereza nchini wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kuongeza tija
na kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe
Magufuli.
Wito huo
umetolewa jana na Naibu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mh John
Mngodo wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa jeshi la hilo
nchini.
“Ni lazima
kil mmoja afanye kazi kwa bidii na weledi
katika eneno lake ili kuongeza tija, kuboresha sekta ya utumishi wa umma
ili kuendana na kasi aliyoanza nayo Rais wa serikali ya awamu ya tano,”alisema
Pia Mngodo
alisema kuwa ni muhimu kwa watumishi wa jeshi hilo kuzingatia nidhamu ya
matumizi ya fedha za umma, utunzaji wa mali za serikali na kupunguza matumizi
yasiyo ya lazima ili fedha zitakazookolewa zitumike katika maeneo mengine ya
kimaendeleo.
Aidha ni lazima kila mtumishi wa umma hususani jeshi la
magereza kuzingatia maadili ya kazi na
kuacha kuomba wala kupokea rushwa ili kuendana na dhamira ya Rais Magufulu ya
‘Tanzania bila rushwa inawezekana’.
Awali katika
hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi Kamishina Jenerali wa Magereza John
Minja alisema kuwa kikao hicho kina lengo la kupokea taarifa ya utekelezaji wa
bajeti ya jeshi hilo katika kipindi cha mwaka wa fedha kuanzia Julai hadi
Septemba mwaka huu.
Aidha kwa
kuzingatia kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano kikao hicho kitatoa nafasi kwa wajumbe wa baraza hilo
kutoa mapendekezo ambayo yatafanyiwa kazi na jeshi la magereza ili kuongeza
tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment