BASATA, TCRA SHIRIKIANENI KATIKA UTENDAJI KAZI

Na Peter Akaro

Baraza la sanaa la taifa(BASATA) ni shirika la umma liloundwa kwa sheria ya bunge namba 23 ya mwaka 1984,BASATA iliundwa ili lisimamie maendelo ya sanaa nchini. BASATA ni chombo chenye uwezo wa hali ya juu wa kutoa huduma bora kitaifa katika maendeleo ya sanaa,kuhimiza na kukuza utamaduni halisi wa sanaa ya kitanzania.

Kwa miaka na siku za karibuni BASATA wamekuwa wakitupiwa lawama nyingi kwa namna wanavyoendesha na kusimamia  shunguli za sanaa nchini.BASATA wamekuwa wa kukurupushwa kila mara,baada ya wadau na mashabiki kupiga kelele kuhusu uteuzi wa Sitti Mtemvu kuwa miss Tanzania mwaka 2013 kuwa iligubikwa na udanganyifu,BASATA waliibuka kutoka usingizini na kuifungia  kwa miaka miwili kamati ya maandalizi ya miss Tanzania.

BASATA wananyooshewa vidole kwa namna maamuzi yao yanavyofanya kazi,kamati ya miss Tanzania iliyofungiwa kwa miaka miwili,baada ya miezi 6 iliondolewa adhabu hiyo nakuruhusiwa kuendekea na shughuli zake,tuachane na hayo.Utakumbuka msanii Shilelo nae alifungiwa kwa mwaka mmoja baada ya picha zake  kusambaa mitandaoni akiwa nusu utupu wakati wa tamasha lake nchini Ubeligiji,lakini msanii huyo alipuuzia adhabu hiyo na kuendelea na shughuli zake na BASATA wakakaa kimya bila kumchukulia hatua yoyote,tuachane na hilo pia.

Kwa sasa mkanganyiko ni mkubwa kwa namna BASATA wanavyofungia kazi za wasanii wa mziki kuchezwa radio na TV,ni kama kumekua mvutano wa pande kuu tatu,BASATA,vyombo vya habari na mamlaka ya mawasilino Tanzania TCRA.

Tazama namna mkanganyiko unavyotokea,msanii anapeleka kazi yake kwenye chombo cha habari ili ichezwe na kuwafikia walengwa,chombo cha habari kinakaa na kutazama maudhui ya kazi ya msanii,na kama imekidhi vigezo vyao wanaicheza.lakini sio ajabu kusikia BASATA wamefungia kazi hii,hili limejitokeza siku chache zilizopita baada ya msanii Ney Wamitego kutoa wimbo wa Shika Adabu Yako,BASATA waliufungia kwa kigezo wimbo huo umejaa matusi,lakini hapo awali vyombo vya habari havikuona hilo,kuna kitengo cha mziki cha radio flani kilisema wimbo huo haukuwa na matusi.

Bado najiuliza kama kituo cha radio kinaweza kucheza wimbo wenye matusi na TCRA wakakaa kimya bila kukichukulia hatua za kisheria kituo hicho, kiueledi wa kazi hili haliwezekani.Mwaka 2014 TCRA waliionya Radio Free Africa baada ya kucheza wimbo wa Nash Mc,ambao walidai ulikuwa na maneno ya uchochezi dhidi ya serikali.

Hapa  utaona kuna umuhimu wa BASATA na TCRA kuwa na mahusiano ya kiutendaji pindi linapokuja swala la kufungia kazi za wasanii kwenye vyombo  habari,na pia vyombo vyote vya habari kupewa muongozo maalumu utakao viwezesha kutokiuka utaratibu.

Siku chache zilizopita nilimsikia Inocent Mongi kutoka TCRA akisema wasanii ni lazima wajue kazi wanazozitoa zinawalenga wa kina nani na kwa muda gani,aliyasema hayo baada ya BASATA kuifungia video ya wimbo wa AY na Diamond-Zigo remix.

Akizungumzia swala  hilo Mongi alisema wasanii wajifunze kutengeneza kazi zenye maudhui mbalimbali,kwani kuna video ambayo huwezi kuitazama ukiwa na watoto na video ya wimbo huo huo unaweza kuitaza ukiwa na mzazi hata watoto.

“Hapa tunatakiwa kuangalia,sawa kuna watu wanapenda hizi nyimbo ndo maana kuna DVD zake ambazo mtu ukinunua zinakua na umri pale,kama ni kwa watu wazima au chini ya hapo, lakini kama unataka upige kwenye radio ambayo itaonekana(kusikilizwa) na hata watoto inabidi sasa uondoe yale mahudhui ambayo yanaweza kukwaza watoto na baadhi ya watu kwenye  jamii.

“Pamoja kuna wengine wanafaidi na kufurahia hicho kitu,kuna wengine pia hawapendi na wanaona wanazalilishwa,kwa hiyo sisi kama mamlaka tunawajibika kwa makundi yote mawili” alisema Inocent Mongi.

Vile vile Mongi aliongeza kuna baadhi ya video kama ile ya AY maudhui yake yanarusu kuchezwa kwanzia saa nne usiku.Huo ulikuwa upande wa TCRA ,vipi kususu COSOTA?.

Chama cha hakimiliki Tanzania COSOTA,nao washirikishwe kwa karibu ili kuondoa mkanganyiko huu,kwanza kila kazi ya msanii kusajiliwa kisheria kabla ya kufikishwa kwenye vyombo vya habari na kwenye jamii,endapo hajaki

No comments: