Na Peter Akaro
Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Buniface Wambura amesema bado ratiba ya ligi kuu imebana hasa kwa timu za Yanga na Azam.
Yanga ambayo inashiriki michuano ya club bingwa Africa inabidi kuhairisha baadhi ya michezo ya ligi kuu,huku Azam wakiwa na viporo vya mechi baada ya kwenda Zambia kwenye michuano maalumu.
Wambura anasema bado hawajui mchezo kati ya Yanga na Mtibwa Sugar utachezwa lini,lakini michezo ya viporo ya Azam imeshapatiwa nafasi.
"Tulifikiria tungepata nafasi wiki hii,lakini wiki hii kuna michuano ya kombe la FA,Yanga wanacheza na vile vile tar 26 Mtibwa wanacheza" alisema Wambura.
Akizungumzia mchezo kati ya Yangu na Azam ambao ndo ulikuwa unafuata baada ya ule wa mtibwa,Wambura alisema bado mchezo huo unatafutiwa nafasi ila bado haijajulikana ni lini utachezwa.
"Unajua mechi za Azam zilikuwa rahisi kuziweka kwa sababu wao hawakuingia katika raundi ya mchujo,lakini kwa upande wa Yanga kwa sababu bado wana mechi za kimataifa bado tunaangalia" alisema Wambura.
Wambura alisema walikuwa wamepanga timu inapomaliza mechi za kimataifa jumatano inacheza mchezo wake wa ligi,lakini kwa sasa kuna ratiba ya FA ambayo kawaida huchezwa wikiendi ya tatu ya mwezi.
"Mfano mechi ya Yanga na Mtibwa tulipanga ingechezwa jumatano hii,lakini unaona jumatano hii ambayo ni tar 24 Yanga anacheza,lakini tar 26 Mtibwa ana mchezo wa FA,kwa hiyo tukawasiliana na TFF,ndo maana utaona mchezo wa FA,kati ya Yanga na JKT Mlale badala ya kuchezwa tar 1,tukawaomba urudishwa uchezwe kesho,alafu tuangalie hapo Yanga wakipata nafasi tuwawekee mechi zao" alisema Wambura.
No comments:
Post a Comment