Na Peter Akaro
Wakati michuano ya CHAN
inayowahusisha wachezaji
wanaocheza ligi za ndani Africa ikifikia
tamati wiki iliyopita nchini Rwanda na
DRC kutwaa taji hilo kwa mara ya
pili,nafikiri Tanzania ina mengi ya
kujifunza kutoka kwenye michuano hii.
Ingawa michuano hii sio maarufu
kama ile ya AFCON,ila ina mchango
mkubwa katika kukuza viwango vya wachezaji wa ndani na hata
kuwatangaza nje ya mipaka ya Africa.
Michuano ya CHAN kwa mwaka
huu naona imebeba jumbe kuu mbili
kwa soka la Tanzania,Kwanza
inatutaarifu tumepotea/kushuka
kisoka,huu ndo ukweli halisi ingawa
TFF ya Malinzi imegoma kumeza
ukweli huu kisa ligi yetu inaoneka
kwenye Tv na uzamini mzuri wa timu ya taifa.
Tumeshuka/kupotea kivipi?,Wakati
CHAN inaanzishwa mwaka 2009
Tanzania tulishiriki kwa mara ya
kwanza katika michuano hiyo
iliyofanyika nchini Ivory Coast.Ilikuwa
ni michuano iliyoshirikisha timu 8
tu,Tanzania ikiwemo chini ya kocha
Mbrazili Maximo,ingawa tulitolea
hatua ya makundi na zambia,tuliamini
tunaelekea katika mafanikio ya soka.
Utakumbuka Tanzania ndo ilikuwa
timu pekee kutoka ukanda wa Africa mashariki na kati kushiriki,kwenye
hatua ya kufuzu tuliwatoa Uganda kisha
Sudan.Leo ni mwaka 2016 wenzetu
Uganda wameshiriki tena kupitia
mgongoni kwetu baada ya kutufunga
hapa nyumbani kisha sare kule kwao.
Tangu kipindi kile hakuna
tunachojivunia katika soka,Ni kama Maximo
alikuwa ameshikilia hatima ya mpira
wetu,Kikosi kile alichokiacha Maximo
ndo kiliiwezesha Tanzania kutwaa kwa
mara ya mwisho ubingwa wa CECAFA
mwaka 2010.Leo Uganda ndo
mabingwa wa CECAFA,ni dhairi wazi
nafasi tuliyokuwa nayo kipindi kile
Uganda wameichukua huku
sinikushuka jamani??.
Ujumbe wa pili kutoka CHAN unasema
ligi yetu sio bora na yenye
ushindani.Wakati michuano hii
inaanzishwa mwaka 2009 DRC
walitwaa ubingwa,kisha mwaka
ulifuata ligi yao ikatoa bingwa barani
Africa ambaye alikuwa ni TP
Mazembe,haikuishia hapo,mwaka
huo huo TP Mazembe wakacheza fainali ya
klab bingwa dunia dhidi ya Inter Milan
na kuwa klabu ya kwanza Africa kufanya
hivyo.
Siri ya mafanikio ya TP Mazembe ni
ubora wa ligi yao na namna
inavyoendeshwa na hata mafanikio ya
DRC kiujumla.Hili ni darasa kwetu na
lazima tujifunze kama tunataka kupiga
hatua kisoka.
Leo TP Mazembe ndo bingwa klab
bingwa Africa na DRC ndo bingwa
CHAN,hakuna cha kushangaza hapa
kwani mipango na misingi yao kisoka
inaruhusu.Mwaka 2010 Spain ulitwa
kombe la dunia,kisha 2012
Barceloona inatwaa UEFA na klab
bingwa dunia,mipango yao na ubora
ligi yao uliruhusu pia.
kama tunaka kufikia mafanikio ya DRC
kwanzia ngazi ya klabu mpaka timu ya
taifa,ni lazima tuache utani na ligi
yetu.Ligi kuu imekuwa ikiendeshwa
kiholela sana hasa upangaji wa
ratiba,vile vile ligi daraja la kwanza
lazima itazamwe kwa jicho la tatu hasa
kashfa za upangaji matokeo.
No comments:
Post a Comment