KABILA AWAFANYIA SURPRISE WACHEZAJI WA NCHI YAKE

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Joseph kabila amewapa zawadi ya magari aina ya Toyota Prado wachezaji wote pamoja na benchi la ufundi la timu ya taifa ya nchi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya timu hiyo kurejea nchini humo ikitokea Rwanda ilipotwaa ubingwa wa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani  maarufu kama CHAN mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumzia zawadi hiyo nahodha wa timu hiyo Joel Kimwaki alisema wamefurahi sana na hawakutegemea kama Rais Kabila angeweza kuwafanyia kitu kikubwa kama hicho.

"Ni kitu cha kushangaza na chakufurahisha pia kwa Rais kutupatia zawadi hii kwani inadhihirisha kuwa amefurahishwa na kazi tuliyoifanya nchini Rwanda na kuliletea sifa taifa letu", alisema.

Aliongeza kuwa tunamshukuru sana kwa moyo wake huo na tunamuahidi kuwa tutaendelea kujituma ili kuzidi kufanya vizuri kwenye michuano mingine zaidi.

Kongo DR siku ya jumapili waliifunga timu ya taifa ya Mali kwa jumla ya mabao 3-0 na kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa Mara ya pili kwenye historia ya michuano hiyo.

No comments: