DIAMOND, MAUA, BEN PAUL WAMVUTIA HERMY B


Na Peter Akaro

Producer kutoka B'Hit's Music
Group,Hermy B amesema kuna
wasanii wa Bongo Flava anatamani
kufanya nao kazi iwapo watakuwa
tayari,kwa haraka haraka Hermy B
aliwataja Maua Sama,Ben Paul pamoja na
Diamond Plutinumz.

Hermy B alisema kitu kilichomvutia
kutoka kwa Maua Sama ni ubora wa
sauti yake kwa sababu yeye akiwa
studio huwa anawarekebisha wasanii
kutoa sauti ambayo yeye anataka
kuisikia vinginevyo hatoweza
kukuruhusu kurekodi.

"Kwa hiyo Maua tukikaa studio labda
tutapambana au kugombana ila
mwishoni tutatoa kitu kizuri" alisema
Hermy B.

Kwa upande wa Ben Paul Hermy B
alisema hajawahi kufanya kazi na
msanii huyo labda kutokua karibu ila
huwa wanakutana na kusalimiana ila
hawajawahi kuwa karibu mpaka
kufanya kazi.Ila Hermy B aliweka wazi
nyimbo inayofuata kutoka kwenye
mikono yake atakuwepo mkali huyo
wa R&B,Ben Paul.

Akimzungumzia Diamond
Plutinumz,Hermy B alimtaja kama
msanii mwenye sauti ya pekee na vile
anavyoweza kuitumia.Vile vile Hermy
B aliongeza Diamond anakitu cha
pekee ambacho watu wengi
hawajui,Diamond ni rapper.

Hermy kwa sasa ana nyimbo mbili
alizotengeza zinazofanya vizuri katika
vituo vya radio na TV,nyimbo hizo ni
Asanteni kwa Kuja ya Mwana FA na
Zigo ya AY aliyoshirikiana na wenzake
Marco Chali na Nahrel kuikamilisha.

No comments: