Na Peter Akaro
Baada ya stori kusambaa kwenye
mitandao ya kijamii kuwa gari la
aliyekuwa miss Tanzania Mwaka 2006
Wema Sepetu linashikiliwa na maofisa
wa TRA,leo hii mrembo huyo
ameibuka na kuzungumzia swala hilo.
Wema Sepetu hakukanusha stori hizo
ila alisema gari ni lake amenunua na
anachosubiri ni kukamilisha usajili tu
lipate namba za Tanzania ila anze
kulitumia.
"Sasa hivi TRA ni waangalifu,hata
hapa sasa hivi kuna rafiki yangu
amekamatwa kwa sababu gari lake
lina namba za Afrika Kusini.
"TRA walinifata wakitaka nyakara za
kumiliki gari,nilipowaonyesha
waliniachia na sasa gari langu lipo
nyumbani" alisema wema.
Vile vile mrembo huyo alisifia utendaji
kazi wa rais Magufuli kwa namna TRA
wanavyochapa kazi.
No comments:
Post a Comment