Na Peter Akaro
Mmiliki wa kiliniki ya tiba asili ya Fore
Plan ameibuka na kukanusha uzushi
ulionea kuwa amefungiwa na serikali
kutoa huduma baada ya Naibu Waziri
wa afya,maendeleo ya
jamii,jinsia,wazee na watoto,Hamisi
Kingwangala kufanya ziara ya
kushtukiza katika kliniki hiyo mwishoni
mwa mwaka jana.
Dk Mwaka alisema uzushi umekuwa
ukienea hasa kwenye mitandao ya
kijami lakini ukweli ni kwamba tangu
tar 21 mwezi wa 12,ambapo
Mheshimiwa waziri alitembelea kituo
chake shughuli ziliendelea kama
kawaida hapakuwa na chochote
ambacho kilitokea kinyume na
utaratibu halisi na shughuli.
"Kuna maelezo yalitolewa awali na
naibu waziri ambayo yalizuia baadhi
ya vitu na kuelekeza vingine lakini
baada ya muda tulikaa chini wa waziri
mwenye dhamana Ommy
Mwalimu,tukazungumza na kujadili
baadhi ya changamoto na njia ya
kuzitatua na baada ya hapo akaja na
tamko lingine ambalo linaloelekeza
watu(matabibu) kusajiliwa,vituo
kusajiliwa jambo ambalo huwezi
kuendesha shughuli zako bila
kulitimiza" alisema Dk Mwaka.
Vile vile aligusia swala la matangazo
yake kustishwa,kwa kusema
matangazo yanafanywa kwa mujibu
wa sheria namba 23 ya mwaka 2002
ya tiba asili na tiba
mbadala,inayosema matangazo yote
kwa ajili ya kumtangaza mganga na
huduma zake ni lazima yapitie baraza
la tiba asili na tiba mbadala,yapewe
kibali ndio yaende hewani.
Dk Mwaka alieleza kusikitishwa kwake
baada ya matabibu kuzuiwa kutoa
elimu wakati matangazo ya tiba asili na
tiba mbadala yanaruhusiwa,Dk Mwaka
alisema huwezi kumtangazia mtu kitu
ambacho huwezi kumuelimisha,yani
inakuwa unamuuzia mbuzi kwenye
gunia,lakini anaamini wamefanya
hivyo
ili kuweka utaratibu mzuri ambao
watu watatoa elimu nzuri ambayo
haitawaadhiri Watanzania kwa ujumla.
Katika mazungumzo hayo Dk Mwaka
ilibidi azungumzie kiwango chake cha
elimu katika tiba asili na tiba mbadala
ili kukanusha uzushi ulikuwa umeenea
kwa muda hasa kuhusu elimu yake.
"Mimi nilianza kwa wazee
wangu,nimefanya kazi za uganga kwa
zaidi ya miaka 15,lakini baada ya hapo
nikaacha nikafanya shughuli zangu
nyingine za IT,baada ya hapo
nikajifunza shughuli za uganga katika
chuo cha Australian Herbal Medicine
(Australia) lakini nikafanya China
mwaka
mmoja,baada yakupeleka vyeti vyangu
baraza la tiba asili na mbadala
wakanibadilishia usajili,nilikuwa
nimesajili kama mganga wa tiba
asili,ila baada ya kupeleka vyeti ndo
nikasajiliwa kama mganga wa tiba
mbadala"alisema.
Kuhusu tuhuma kwamba kituo chake
kimekuwa kikitumia mashine za kisasa
wakati ni cha tiba asili,Dk mwaka
alisema kuna baadhi mashine
zinaruhusiwa katika tiba asili lakini
mashine kama CT Scana wao
hawana.Dk Mwaka aliongeza kwa
kusema tatizo kumekuwa na baadhi
ya watu hawana tahaluma ya kutosha
kutumia hivyo vifaa na wanalazimisha
kuvitumia na hatimae wanashindwa
kutoa majibu na maelekezo sahihi kwa
wagonjwa kitu ambacho kimeleta
mgogoro.
Dk Mwaka alieleza namna kitu chake
kinavyopata vipimo sahihi kutoka kwa
wagonjwa kwa kusema.
"Kwanza wangonjwa wanapokuja
kwangu,achilia mbali mafaili
anayokuja nayo toka hospitali
mbalimbali,yeye mwenyewe kichwani
kwake ana faili zima,sasa mimi
anapoelezea pale maelezo yake
yanatosha kusema sasa huyu
nimfanyie kipimo gani ili nijiridhishe
kwa njia zangu nimsaidieje.
"Lakini kwa bahati mbaya sana au
nzuri niseme serikali ipo katika
mchakato wa kuhakikisha kuna kuwa
na 'medical reference' mchakato ambao
unaendelea utachukua muda kidogo
lakini naamini itafika hatua utakuwa
sawa,kwa sababu ni ukweli
usiopingika wagonjwa wanakuja kwetu
na wagonjwa wanatoka kwetu
tunawarudisha hospitali" alisema Dk
Mwaka.
No comments:
Post a Comment