DSJ WALIPA KISASI KWA TSJ

Na Peter Akaro

Timu ya mpira wa miguu ya chuo cha uandishi wa habari
TSJ,walijikuta wakiambulia kipigo kizito
cha mabo 3 kwa 1 kutoka kwa majirani na mahasimu wao wakubwa  DSJ
katika mchezo wa kujipima ubavu
uliochezwa katika viwanja vya bonde la mto msimbazi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika mchezo huu ambao ulianza
kwa kasi kwa timu zote mbili kutafuta
goli la mapema,TSJ ndo walikuwa wa
kwanza kuchungulia lango la DSJ
kupitia mchezaji wake Tobias
aliyekwamisha mpira wavuni dk 10
lakini muamuzi alilikataa goli
hil.

Iliwachukua dk 14 DSJ kuandika
goli la kwanza kupitia mshambulia
wake Mudy aliyetumbukiza mpira wa
adhabu wavuni baada ya TSJ kucheza
madhambi,mpaka kipindi cha kwanza
kinamalizika DSJ walikuwa mbele kwa
goli moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi hasa
kwa upande wa TSJ waliobisha hodi
mara kwa mara langoni mwa DSJ
wakitaka kurudisha goli, kunako dk 55
nahodha wa TSJ Prosper Kaijage  alitumbukiza
mpira wavuni na kufanya ubao wa
matangazo kusomeka 1-1,
bao hilo liliwarudisha TSJ mchezoni
na kutaka kuongeza goli lakini ubutu
na ukosefu wa umakini wa safu ya
ushambuliaji uliwakwamisha,dk 67
Amiri alishindwa kuiandikia TSJ goli la pili baada ya kuwatoka vema walinzi wa DSJ.

Kunako dk 71 DSJ waliwainua
mashabiki wao baada ya kujiandikishia
goli la pili kupitia mshambuliaji wake
Jerry, hali ilianza kuwa mbaya kwa TSJ
kunako dk 73 baada ya mchezaji wake
Elia kuumia na kutolewa nje kupatiwa
huduma ya kwanza lakini hakuweza
kuendelea na mchezo.

Jahazi la TSJ lilionekana wazi
limeridhia kuzama baada ya
kumruhusu mshambuliaji DSJ Romeo
kwenda kuokuta mpira wavuni kunako
dk 79,bao hilo liliibua shangwe,kelele
na vifijo uwanjani hapo kutoka kwa
mashabiki wa DSJ,huku upande wa
TSJ wakiwa wametulia kama maji ya mtungi.

Mpaka muamuzi anapuliza kipenga
kuashiria dk 90 za mchezo
zimemalizika,ubao wa matangazo
ulisomeka DSJ 3 na TSJ 1.

MANAHODHA WAZUNGUZA.
Baada ya mchezo huo kumalizika mwandishi wa habari hii alifanikiwa kuzungumza na
manahodha wa timu zote mbili kutaka
kujua tasmini ya mchezo
huo.Nahodha wa DSJ Michael alisema
mchezo ulikuwa mzuri kiujumla
ikizingatia mchezo wa kwanza
walipoteza kwa bao 7 kwa 1 kwaihiyo wanafurahi kulipa kisasi japo sio kwa idadi ile ya mabao.

"Japokuwa wengi ni wageni ndo
tumekuja semista ya kwanza,sisi
tulikuwa hatujui hii timu,tumekuja
tumejipanga kwa moyo mmoja
pamoja na kufuta makosa yetu ndo
tukashinda" alisema Michael.

Nahodha wa TSJ Prosper Kaijage  ambae ndio
alifunga goli la kufutia machozi kwa
timu hiyo,alisema wanakubaliana na
matokeo kwa kuwa mchezo una vitu
vitatu(kushinda,sare na kufungwa).

"Ila timu yetu ilikuwa na wachezaji
wengi wageni,hivyo tulikuwa
tunapanua ukubwa wa kikosi lakini
tumeona matokeo yake,kwa hiyo
nafîkiri tutajindaa zaidi kwa ajili ya
mazoezi zaidi,na bila shaka tutapata
matokeo kwa sababu matokeo ya
kwanza tulishinda goli 7 kwa 1,ila sasa
hivi tumepoteza 3 kwa 1,ni moja kati ya
mchezo" alisema Prosper.

NIDHAMU YA MCHEZO KIUJUMLA.
Mchezo ulikuwa wa kiungwana hasa
kipindi cha kwanza,lakini kipindi cha
pili kunako dk 76 ya mchezo kuliibuka
ugomvi kati ya Gowele wa TSJ na
Romeo wa DSJ,baada ya Gowele
kumkwatua kwa makusudi Romeo ili
kulipiza kisasi.
Ugomvi huu ulipelekea mchezo
kusimama kwa muda huku muamuzi
na wachezaji wa timu zote wakiamua
ugomvi wa wawili hao waliotaka
kuzichapa kavu kavu uwanjani
hapo,lakini baadae hali ilitulia na
mchezo kuendelea.

No comments: