Watu saba wameripotiwa kufariki Dunia jijini Dar es salaam kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbailimbali nchini.
Wawili kati ya watu waliofariki vifo
vyao vimetokana na kukanyaga nyaya za umeme ambazo zilikua kwenye maji baada ya kuanguka kwa nguzo ya umeme na wengine wamefariki kutokana na kuzidiwa na
nguvu ya maji katika eneo la Buguruni kwa myamani jijini Dar es salaam.
Hii sio mara ya kwanza kwa mvua za
masika kusababisha vifo vya watu kwani takribani miaka miwili ilopita mvua hizo
zimekuwa zikisababisha maafa makubwa ikiwemo vifo pamoja na kuwaacha watu
wakiwa hawana mahali pakuishi.


No comments:
Post a Comment