Waziri mkuu wa zamani ambae pia ni
mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowasa amesema uvumi ulioenea kuwa makundi
mbalimbali yakiwemo ya viongozi wa dini yanayojitokeza kumshauri
atangaze nia ya kugombea nafasi ya uraisi katika uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka
huu kuwa sio kweli na yeye hana uwezo wa kuyalipa makundi yote hayo
Lowasa amesema kuwa hizo ni taarifa
za kipuuzi kwani yeye hana uwezo wa kuyalipa makundi hayo, pia ameongeza kuwa
watu hao wana imani naye na wanamapenzi na nchi yao.
Mbunge wa jimbo la Monduli Edward Lowasa
No comments:
Post a Comment