Serekali kupitia Waziri wa fedha Mh
Saada Mkuya leo imewasilisha bungeni muswada wa sheria ya mfumo wa malipo ya
mwaka 2015 huku wabunge wengi wakizungumzia swala la wizi wa mtandao kua ni
changamoto na tatizo kubwa katika swala zima la malipo ya kimtandao
Waziri wa fedha Mh Saada Mkuya
Wakichangia katika muswada huo mapema
leo jioni baadhi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania
wamesema kuwa wizi wa mtandao ni swala lilnalotakiwa kupewa kipaumbele katika
muswada huo kwani limekuwa likiwatesa sana wananchi.
Muswada huu utakuwa ni muswada wa nane kuwasilishwa na
serekali katika bunge hili la kumi baada
ya Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa
Ajira za Wageni wa Mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa Mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa Mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Usimamizi
wa Kodi wa Mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2014, Muswada wa
Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa Mwaka 2014 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya
Sheria ya Stakabadhi Ghalani wa Mwaka 2014,
.jpg)
.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment