Jeshi la polisi mkoani rukwa linawashikilia watu saba hadi sasa, kwa
tuhuma za kuhusika na kitendo cha kikatili cha kukata kiganja cha mkono
wa kulia, cha mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Baraka Cosmas Lusambo mwenye
umri wa miaka sita, katika kitongoji cha kikonde kata ya kipeta wilaya
ya sumbawanga vijijini, ambapo pia katika tukio hilo wamemjeruhi mtoto
huyo mkono wa kushoto.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa rukwa kamishna msaidizi wa polisi
Leons Rwegasira, amesema wamefanikiwa kuwakamata watu hao kufuatia msako
mkali, mara tu baada ya kutokea tukio hilo kwenye kitongoji hicho cha
kikonde, ambacho kinakuwa na wakazi wakati wa msimu wa kilimo na
kiangazi watu wanahama tena, katika familia yenye watoto wengine watatu
wenye ulemavu wa ngozi
Mtoto baraka na mama yake mzazi wamelazwa kwenye hospitali ya rufaa
ya jijini mbeya, wakitibiwa majeraha waliyoyapata wakati wa purukushani
za kumshambuliwa mtoto huyo.
.jpg)
No comments:
Post a Comment