Mkazi mmoja wa Moshi mkoani Kilimanjaro Abedi Abdullahi amekutwa akiiishi na watoto wapatao kumi na
saba akiwa amewahifadhi kinyume cha sheria katika nyumba yake kwa madai
kuwa anawafundisha elimu ya dini ya kiislam.
Akizungumzia jinsi anavyoishi na watoto hao Abedi Abdullahi amesema
asilimia kubwa ya watoto hao ni ndugu kutoka familia mbalimbali ikiwemo
kutoka Moshi na Mwanza na kwamba anawafundisha elimu ya dini ya kiislamu
ambapo wazazi wa watoto hao wameridhia jambo hilo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga
Mkuu wa wilaya ya Moshi Novatus Makunga amesema kwa sasa watoto hao
wameondolewa katika eneo hilo na kurudishwa kwa wazazi wao huku
mahojiano na uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukiendelea.
Ramadhani Mohamed ni mkazi wa Matindigani ambaye ni mmoja wa wazazi wa watoto watatu kati ya hao ambapo amedai kupotelewa na watoto wake tangu februari mwaka jana

No comments:
Post a Comment