Waziri wa maliasili na utalii Mh Lazaro Nyalandu leo amepokea ndege aina ya Micro Light Nyinja 5H- HEL kutoka kwa kampuni inayojihusisha na maswala ya utalii ya Tanganyika Wildlife Safari itakayosaidia katika harakati za kupambana na uuaji na ujangili kwa wanyama pori nchini
Akipokea ndege hiyo jijini Dar es salaam Waziri Nyalandu alisema ndege hiyo ni mpya kabisa na yausalama wa hali ya juu kutokana na muonekano wake kua wa kisasa zaidi.
"Hii ndege ni salama zadi kwasababu yenyewe imejengwa na parachuti yake endapo kunatokea chochote wakati ikiwa angani inafungua parachuti ambayo itaisaidia yenyewe na watu waliomo hivyo ni yauhakika zaidi" Alisema Waziri Nyalandu
Naye mwenyekiti wa kampuni iliotoa ndege hiyo Eric Pasanisi alisema ndege hiyo inathamani ya dola laki mbili na ishirini elfu na kueleza sifa mbalimbali za ndege hiyo.
Waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu (Kushoto) akikabidhiwa ndege hiyo na mwenyekiti wa kampuni ya Tanganyika Wildlife Safari Eric Pasanisi (Kulia) wengine ni askari wa wanyama pori waliohudhuria makabidhiano hayo
No comments:
Post a Comment