Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Anna Makinda amesema Zitto Zubeir Kabwe bado ni
mbunge halali wa jimbo la Kigoma kaskazini kutokana na spika huyo
kutokupata taarifa rasmi kutoka tume ya taifa ya uchaguzi kuhusiana na
kutengeliwa ubunge huo.
Makinda alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kumi na tisa wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ambao umeanza leo mkoani Dodoma huku serikali ikisema madhaifu yaliyopo katika
jeshi la polisi yamechangia vitendo vya uporaji na uvamizi wa vituo vya
polisi.
Dakika chache baada ya mkutano huo kuanza spika wa bunge
Mhe.Anna
Makinda aliwataka wabunge wasimame kimya dakika moja kumkumbuka
aliyekuwa mbunge wa jimbo la mbinga magharibi kapteni mstaafu John Komba
aliyefariki hivi karibuni
Katika kipindi cha maswali na majibu, naibu waziri wa mambo ya ndani
Pereira Sillima amesema madhaifu yaliyopo kwa baadhi ya askari polisi
yamekuwa yakichangia vituo hivyo kuvamiwa na polisi kuporwa silaha hivyo
ni bora polisi wakajirekebisha.
No comments:
Post a Comment