Jeshi la polisi mkoani Dodoma likishirikiana na wananchi limewakamata wahamiaji haramu 64 raia wa Nchi ya ETHIOPIA (wahebeshi) katika kijiji cha kidoka kata ya kidoka tarafa ya Goma wilaya ya Chemba mkoani wa Dodoma mmoja kati yao akiwa amefariki alietambuliwa kwa jina moja la TAJIRU anaekadiriwa kua na umri wa kati ya miaka 25-30 .
Watu
hao walikuwa wakisafirishwa kwa Lori lenye namba za usajili T.353 AYW
Mitsubishi Fuso lililokuwa likiendeshwa na OTHMAN YUNUS MTEKATEKA, miaka
45, na Mkazi wa ILALA Jangwani jijini Dar es Salaam akitokea Moshi -
Kilimanjaro kwenda mkoani Mbeya.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma(Pichani juu) Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME – SACP amesema Mnamo tarehe 14/03/2015 saa 01:00 asubuhi katika
kijiji cha KIDOKA walionekana watu wengi wasiofahamika wakiwa
wamejificha katika vichaka na mashamba ya watu.
Watu
hao walionekana dhaifu, walikuwa wakila mahindi mabichi na wengine
wakiomba kwa wanakijiji waliokuwa wakipita maeneo jirani msaada wa
chakula na maji ya kunywa kwa ishara, kwa kuwa hawakuwa na uwezo wa
kuongea lugha ya Kiingereza wala Kiswahili.
No comments:
Post a Comment