KESI YA KENYATTA YAFUNGWA ICC

Kesi iliokua inamkabili Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta imefungwa rasmi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC iliyopo The Hague nchini Uholanzi.

Raisi Kenyatta alikua ameshitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.














































Mwezi Disemba kiongozi wa mashtaka alimuondolea mashtaka kiongozi huyo akisema kuwa serikali ya Kenya imekataa kuipatia mahakama hiyo ushahidi muhimu.
Hatahivyo mahakama hiyo imesema kuwa upande wa mashtaka una uwezo wa kuanzisha mashtaka mapya katika siku za usoni iwapo ina ushahidi wa kutosha.





















































Kesi ya makamo wa rais William Ruto inaendelea katika mahakama hiyo baada mawakili wake kushindwa kuiondoa kesi yake.




No comments: