Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi imepanga kuwasilisha
kwenye bajeti ijayo mpango maalum wa kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango
vya kodi ya ardhi ili iweze kulipika na kuwawezesha watanzania walio
wengi, wawekezaji na mashirika likiwemo shirika la nyumba la taifa NHC
kumiliki ardhi.
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, william lukuvi akiongea
jijini mwanza na kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi maliasili na
mazingira kwenye mkutano wa majumuisho ya ziara zilizofanywa na kamati
hiyo katika nchi mbalimbali ikiwemo dubai, afrika kusini, uganda na
ethiopia amesema serikali pia
imejipanga kuhakikisha usimamizi na
umilikaji wa masuala ya ardhi kuwa wa kielektroniki katika nyanja zote
na kuondokana na mfumo wa kizamani wa analog.
Aidha waziri Lukivi amewatoa hofu wananchi wa mji wa kigamboni na
amesema serikali haitanyang’anya ardhi wananchi wa mji huo na wala
haitawalipa fidia badala yake wananchi watakuwa na haki ya kuyaendeleza
maeneo yao wenye au kuingia ubia na wawekezaji kwa mujibu wa utaratibu
uliowekwa au MASTER PLAN ambayo haitasabaisha kero na usmbufu kwa wananchi
Mji wa kigamboni
Wakiongea kwenye mkutano huo wa majumuisho,baadhi ya wabunge
wameipongeza serikali kwa uamuzi huo ambao wamesema utawafanya wananchi
wa kigamboni sasa waishi kwa amani lakini pia wameishauri serikali
kuliwezesha shirika la nyumba la taifa NHC ili liweze kutekeleza
kikamilifu mipango yake ya ujenzi wa nyumba bora na za Gharama nafuu kwa
watu wenye kipato cha chini.



No comments:
Post a Comment