MWILI WA MARSH KUAGWA LEO MUHIMBILI.

Mwili wa aliekua kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars marehemu Sylvester Marsh unatarajiwa kuagwa leo saa sita mchana katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambopo ndipo umauti ulipomkuta.
















Enzi za uhai wake Marehemu Syvester Mash (kushoto) akipewa maelekezo toka kwa aliyekuwa kocha wa timu ya Tanzania Taifa Stars Kim Poulsen


Mwili huo unatarajiwa kuagwa leo majira ya saa sita mchana kisha kusafirishwa kueleka jijini Mwanza  amboko ndipo mazishi yanapotarajiwa kufanyika


Marehemu Sylvester Marsh (wa pili kutoka kushoto) akiwa na viongozi wengine wa Taifa Stars enzi ya uhai wake.


Marehemu  Sylvester Marsh alifariki jana alfajiri katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ambako alikua amelazwa akiwa anasumbuliwa na matatizo ya kansa ya koo 
















Buriani Sylvester Marsh, utakumbukwa daima kwa mchango wako katika soka ya Tanzania

Marsh alianza kuwa Kocha Msaidizi wa timu za vijana Tanzania ikiwemo Serengeti boys,Kilmanjaro stars,pia kafundisha Kagers Sugar(2005-2008),94 KJ,Toto African na kocha mkuu wa Mwanza Queens(2015) .
Kocha Marsh pia alikuwa kocha Mkuu wa timu yake ya Marsh Athletics ya Mwanza iliyopo Ligi Daraja La tatu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amin.








No comments: