Mbunge wa Kigoma kaskazini Mh.Zitto Kabwe ametangaza rasmi kutogombea
tena ubunge katika jimbo hilo baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka
huu, huku akiwashukuru wananchi wa jimbo lake kwa kumpa dhamana ya
kuwawakilisha bungeni kwa kipindi cha miaka 10 licha ya kukutana na
vikwazo vingi.
Akiongea na wapiga kura wake hao Zitto amesema kwa kipindi chote akiwa
mbunge alijitahidi kwa kadri alivyoweza kutetea si tu maslahi kwa watu
wa jimbo lake bali kwa taifa zima kwa ujumla na kwamba ataendelea
kufanya hivyo kama raia ili kuondoa kila aina ya ufisadi na kutumia
rasilimali za nchi kuondoa umasikini, ujinga na maradhi.

.jpg)


No comments:
Post a Comment