Mradi wa ujenzi wa Dampo la Kisasa unaotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la MBEYA
kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 3.7 umekamilika tayari , mradi huo utapunguza mlundikano wa taka ngumu na sumu kuzunguka mji wa MBEYA.
Afisa Mkuu wa Idara ya Mazingira wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya SAMWEL
BUBEGWA amemwambia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Dr
BINILITHI MAHENGE kuwa mradi huo unafadhiliwa na benki ya
dunia,kinachosubiriwa ni magari ya kubebea taka na vishimba zaidi ya 90
kuwasili kutoka nchini afrika ya kusini.
Mradi huu unakamilika huku kukiwa na utekelezaji wa agizo la Makamu wa
Rais la kufanya usafi wa mazingira kila jumamosi,hata hivyo Waziri wa
Nchi ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Dokta BINILITHI MAHENGE
anawakumbusha wakurugenzi watendaji wa wilaya, miji na majiji kuanza
rasmi kutenga bajeti za usafi wa mazingira katika maeneo yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamuu wa Rais mazingira Amehitimisha ziara
mkoani Mbeya kwa kugakua kiwanda cha saruji cha Songwe,kilichopo nje
kidogo ya Jiji la Mbeya, kiwanda hiki kimekuwa kikilalamikiwa na baadhi
ya wananchi juu ya athari za uchafuzi wa mazingira zinazotokana na
uzalishaji wa saruji ambalo tatizo kubwa ni vumbi na moshi.




No comments:
Post a Comment