WATATU MBARONI KWA KUHUSIKA NA TUKIO LA KUMDHURU SLAA

Jeshi la polisi mkoani DSM limewakamata na kuwafikisha mahakamani watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na kusudio la kumdhuru Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA Dkt WILBROAD SLAA na mlinzi wake KHALID KAGENZI. 













Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya DSM SULEIMAN KOVA 


















Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya DSM SULEIMAN KOVA amewambia waandishi wa habari kuwa watuhumiwa ni maafisa ndani ya chama hicho katika ngazi tofauti ambao shauri lao litafikishwa kwa Mwanasheria wa serikali Kanda ya DSM kwaajili ya kutolewa maamuzi. 

















Wilbroad Slaa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)













Pia KAMISHNA KOVA amesema sheria na tararibu uwazi utazingatiwa katika kutenda haki.

Watuhumiwa wote watatu wapelekwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi yao itatajwa tena MACHI 26 mwaka huu.

Katika hatua nyingine Kamishna KOVA amesema polisi inamshikilia HARUBU MTOPA Mkazi wa MBAGALA kwa tuhuma za kujipachika cheo cha Katibu wa Rais JAKAYA KIKWETE, PROSPER MBENA.

























No comments: