NI VITA ROBO FAINALI KOMBE LA FA LEO

Manchester united leo itakua nyumbani Old Traford kuwakaribisha Arsenal katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya kombe la FA.



Mechi hiyo inayotarajiwa kuanza majira ya saa tano kasorobo kwa saa za Afrika mashariki inatarajiwa kua ya kuvutia kutokana na historia ya timu hizo katika michuano ya kombe la FA


Timu hizo zimekutana mara 21 katika kombe la FA huku Man U wakishinda mara 13 Arsenal wakishinda mara 7 na wakitoka sare mchezo mmoja 
Mara ya mwisho timu hizo kukutana katika michuano hiyo ilikua Disemba mwaka 2011 kwenye raudi ya sita ya kombe hilo ambapo Manchester Unite walishinda kwa mabao mawili kwa sifuri mabao yaliyofungwa na Wayne Rooney pamojoja na Fabio Da Silvaa 

Fabio Da Silva akishangilia goli alilofunga dhidi ya Arsenal kwenye mechi ya raundi ya sita ya kombe la FA Disemba mwaka 2011









No comments: