ACT WAJIGAMBA KUNYAKUA MAJIMBO MANNE KWENYE UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU

Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT)  kimesema kuwa kinatarajia kunyakua majimbo manne ya ubenge katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu




















Akizungumza katika kipindi cha Hot Mix kinachorushwa na kituo cha EATV kiongozi mkuu wa chama hicho Zitto Zuberi Kabwe alisema majimbo wanayaotarajia kuyachukua katika uchaguzi mkuu mwaka huu ni pamoja na jimbo la Ubungo linaloongozwa na John Mnyika (Chadema), jimbo la Kawe linaloongozwa na Halima Mdee (Chadema), jimbo la Segerea linaloongozwa na Makongoro Mahanga (CCM) na jimbo la Kahama linaloongozwa na James Lembeli (CCM).


"Nina maombi jimbo la Kawe, Ubungo, Segerea pamoja na Kahama lakini kwa kuwa ACT kinaongozwa kizalendo, tutaweka utaratibu mzuri wakuweka wagombea kila eneo " Alisema Zitto.
Hata hivyo Zitto aliendelea na msimamo wake wa kutogombea tena ubunge kwenye jimbo aliliokuwa analiongoza alipokuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema la Kigoma Kaskazini


"Kwa mimi binafsi siwezi kusema kuwa wapi nitagombea ila sitagombea tena jimbo la Kigoma Kaskazini" Alisema Zitto.





No comments: