SHIPOLOPOLO KUTUA LEO TAYARI KWA KUIKABILI TWIGA STARS

Timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Zambia (shipolopolo) inatarajiwa kuwasili leo hapa nchini kwaajili ya kuikabili timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) kwenye mechi ya marudiano ya kusaka tiketi ya kushirika michuano ya  Afrika kwa upande wa wanawake itakoyafanyika nchini Congo Brazzaville Septemba mwaka huu.




 Katika mechi ya awali iliopigwa kwenye uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka nchini Zambia wiki mbili zilizopita timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) iliibuka na ushindi wa magoli 4-2. Kwa matokeo hayo Twiga Stars inayonolewa na kocha Rogasian Kaijage inahitaji sare au ushindi wa aina yoyote ili iweze kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo



Mechi hiyo ya marudiano inatarajiwa kuchezwa siku ya ijumaa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kama ilivyo kawaida timu ya Shipolopolo inayonolewa na kocha Albert Kachinga  itapata nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja huo ili iweze kuzoea mazingira ya uwanja.


No comments: