AJALI YAUWA 10 TANGA

Watu kumi wameripotiwa kufariki Dunia papo hapo kwenye ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la mkata wilaya ya handeni mkoani Tanga.





Kamanda wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga amesema kuwa ajali hiyo imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar es salaam kwenda Tanga na Arusha.


Kwa mujibu wa Kamanda gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokua mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.



Baada ya Basi la Ratco kugongana na gari ndogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngorika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha.

Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia wanaume watano wakiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi la Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.




No comments: