Jeshi la polisi jijini Dares salaam wamelazikmika kutumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu zinazofanywa na abiria pamoja na wananchi kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha ubungo kufuatia mgomo wa madereva wa daladala pamoja na mabasi yanayoenda mikoani na nchi jirani ulioanza mapema asubuhi ya leo.

Mgomo huo ambao unafanyika nchi nzima umekuja kufuatia madereva kutaka kuwekewa mazingira mazuri katika kazi yao ikiwemo kupewa mikataba mizuri na wamiliki wa vyombo hivyo pamoja na kuishinikiza serekali ifute utaratibu wa kutaka madereva warudi vyuoni kusoma kwa mara nyingine mara tu baada ya leseni zao kuisha mda wake.
Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha jinsi hali ilivyokuwa kwenye baadhi ya vituo mbalimbali vya mabasi jijini Dar es salaam ikiwemo stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na cnhi jirani Ubungo kutokana na mgomo wa madereva ulionza leo asubuhi katika mikoa mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment