HATIMAYE SERIKALI YAKUBALIANA NA MADAI YA MADEREVA NCHINI

Serikali imekubali kufuta utaratibu wa kuwataka madereva kusoma upya kwenye chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) mara tu baada ya kuisha kwa muda wa leseni zao


waziri wa kazi na ajira Mh Gaudencia Kabaka


Akizungumza na baadhi ya madereva kwenye stendi kuu ya mabasi
 yaendayo mikoani (Ubungo) mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichowahusisha madereva, wamiliki wa mabasi pamoja na serikali kilichofanyika Ubungo waziri wa kazi na ajira Mh Gaudencia Kabaka alisema kuwa serikali imekubali kufuta utaratibu huo wakuwataka madereva kwenda kusoma kila baada ya leseni zao kuisha muda wake.


Hatua hiyo imekuja mara baada ya madereva kutoka maeneo mbalimbali nchini kugoma na kuishinikiza serikali kuondoa utaratibu wa kuwataka madereva kuanza kusoma baada ya leseni zao kuisha muda wake na kutaka kuwekewa mazingira mazuri kwenye kazi yao.


Nae kwa upande wake kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam Kamishina Suleimani Kova wakati akizungumza na madereva hao aliwaahidi kuwa ataondoa utarati wa kuweka vipima spidi maarufu kama Tochi kwenye maeneo mbalimbali ambayo nayo nimoja ya kero kwa madereva hao.

Uamuzi wa serekali umefanya hali ya usafiri kurudi katika hali ya kawaida mara baada ya madereva kukubali kusitishi mgomo na kuendelea na kazi kama kawaida.

No comments: