APC CHAENDELEZA USHINDI NIGERIA

Chama cha rais mteule wa Nigeria The All Progressives Congress (APC), kimepata ushindi mkubwa wa majimbo 19 kati ya 29 katika matokeo ya hivi punde yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi INEC.


Awali INEC ilikuwa imethibitisha kuwa chama cha rais mteule The All Progressives Congress (APC) kilikuwa kimetwaa miji mikuu ya Lagos Kaduna na na Katsina.
Matokeo haya ya hivi punde ni dhihirisho kuwa raia wa Nigeria walipigia Kura kiongozi wa upinzani Jenerali mtaafu Muhammadu Buhari.
Ushindi huo ni dhidirisho ya kuwa chama kinachoondoka madarakani cha Rais Goodluck Jonathan PDP kimepata matokeo mabaya  zaidi tangu kukamilika kwa utawala wa kijeshi mwaka wa 1999.














Uchaguzi huu wa majimbo umeendeleza dhana ya kuwa APC itazoa maeneo wakilishi mengi kufuatia ushindi wa kihistoria wa jenerali mstaafu Muhammadu Buhari.
Siku ya jumapili, tume huru ya uchaguzi nchini humo (Inec) ilitangaza rasmi kuwa chama cha Jenerali Buhari APC ilikuwa imetwaa jimbo la Lagos mbali na kushinda ugavana wa majimbo ya Kaduna na Katsina majimbo


Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari anatarajiwa kuapishwa rasmi kama rais wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika mwishoni mwa mwezi Mei.



No comments: