ZUMA AWATEMBELEA WAATHIRIKA WA GHASIA

Raisi wa Afrika ya kusini Jacob Zuma amewatembelea na kuwaomba raia wa kigeni walioathirika na vurugu zinazoendelea nchini humo  kubaki nchini humo wakati alipositisha ziara yake ya kiserikali nchini Indonesia ili kushuhulikia wimbi hilo la chuki dhidi ya wageni.


Ghasia hizo ambazo zilianza wiki tatu zilizopita zimesababisha watu 6 kufariki dunia na wageni 5000 kuyakimbia makazi yao na kutafuta hifadhi katika kambi za muda 



Machafuko hayo ambayo yalianzia mji wa mshariki wa Darban kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi hiyo yanabeba hisi za chuki dhidi ya wageni ambazo ziliikumba Afrika ya Kusini mwaka 2008 yaliyosababisha vifo vya watu 62.



"Kama serikali , hatuwaambii nendeni zenu". Sio kila raia wa Afrika kusini anasema , nendeni zenu". Ni idadi ndogo sana ya watu ambao wanasema hivyo," Zuma amesema katika kambi ya Chatsworth, ambako alikabidhi hundi ya dola 4,100 kuwasaidia wahanga wa ghasia za chuki dhidi ya wageni.


Ameahidi kumaliza ghasia hizo na alilihakikishia kundi hilo la watu kwamba kuna nafasi kwa wageni nchini Afrika kusini. "Hata kama kuna wale wanaotaka kurejea nyumbani, wafahamu kwamba wakati tutakapositisha ghasia wanakaribishwa kurejea, " Alisema Zuma
































Nae kwa upande wake Rais wa  Zimbabwe Robert Mugabe ameyalaani vikali machafuko hayo nakusema kuwa ameshtushwa na kuchukizwa na ghasia hizo.














No comments: