HIVI NDIVYO ILIVYOKUA UGAWAJI WA ZAWADI ZA LIGI KUU MSIMU WA 2015/2016

Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom ambao ndio wadhamini wakuu wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara kushirikiana na shirikisho la soka nchini TFF jana usiku walitoa zawadi mbalimbali za ligi hiyo kwa msimu wa mwaka 2015/2016 ambao umemalizika kwa klabu ya yanga kuibuka mabingwa.

Katika hafla hiyo iliyofanyika jana usiku kwenye hoteli ya Jb belmount iliyopo posta jijini Dar es salama mgeni rasmi alikua ni Naibu waziri wa wizara ya habari utamaduni na michezo mh Juma Nkamia zawadi mbali zilitolewa kama vipengele vilivyokua vimepangwa.

Baadhi ya zawadi zilizotolewa jana usiku ni pamoja na timu bingwa ambayo ni klabu Yanga ilipokea hundi ya kitita cha shilingi milioni 80.
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja Simon Msuva alipokea zawadi ya mfungaji bora, shabani kado akipata zawadi ya golikipa bora huku kwa upande wa kocha bora zawadi hiyo ikienda kwa kocha Mbwana Makata wa timu ya Prison ya mbeya.

Hizi ni baadhi ya picha za jinsi ilivyokua jana usiku kwenye ugawaji wa zawadi hizo.

No comments: